Mratibu wa bahati nasibu ya Movie Leo ambaye ni mtangazaji wa Clouds FM, Zamaradi Mketema (kushoto) akikabidhi ufunguo wa pikipiki Dar es Salaam jana kwa mshindi wa tatu wa bahati nasibu hiyo, Hassan Ahmed kutoka Tanga.
MKAZI wa Tanga, Hassan Ahmed jana alikabidhiwa pikipiki aina ya Toyo baada ya kushinda bahati nasibu inayoendeshwa na kituo cha redio cha Clouds FM na Kampuni ya kusambaza filamu ya Steps Entertainment kupitia kipindi cha Movie Leo cha Clouds.
Mratibu wa bahati nasibu hiyo ya kununua filamu halisi badala ya za kughushi, Zamaradi Mketema ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Movie Leo, ndiye alikabidhi pikikipiki hiyo kwa mshindi, Dar es Salaam jana.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Zamaradi alisema Clouds FM inashirikiana na Steps Entertainment kuendesha bahati nasibu hiyo ambayo mshindi anapata pikipiki inayotolewa na kampuni ya Kishen Enterprises.
Bahati nasibu hiyo ilianza Januari 5, mwaka huu na Hassan ni mshindi wa tatu aliyeshinda katika ununuzi wa filamu za April Fool, Ganzi la Moyo, Shetani wa Pesa na Wrong Number ambazo kuponi zake za ushiriki zinapatikana nyuma ya nakala halisi ya filamu.

0 comments:
Post a Comment