Kamishna wa jeshi la polisi Paul Chagonja akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kutokana na milipuko iliyotokea katika Ghala la Jeshi katika kambi iliyoko mbagala Zhakhem, Kamishna Chagonja akiwa katika eneo la tukio amesema wananchi wawe watulivu wakati jeshi hilo pamoja na Jeshi la wananchi JWTZ wakishirikiana kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzima moto unaowaka, Chagonja amesema watu wasisogee eneo la tukio kwani bado si salama kutokana na milipuko kuendelea kusikika mpaka hali itakapokuwa imetulia ameongeza kuwa ni mapema kueleza chanzo cha milipuko hiyo na hasara yake au madhara yaliyotokea kwa bidadamu, lakini wananchi wawe watulivu watapewa taarifa.
Askari wa jeshi la ulinzi wakifukuza raia wasisogee karibu na eneo la tukio kwa usalama wao, hata hivyo watu wengi waliofika kutaka kushuhudia tukio hilo walikuwa wabishi kuondoka, kana kwamba hawajui madhara wanayoweza kuyapata kutokana na milipuko hiyo.
Na hivi ni vipande vya mabomu vilivyotua mbagala kizuiani baada ya mlipuko kama unavyoona wakazi wa maeneo hayo wakivishangaa.
Hiki ni moja ya kipande cha bomu kilichoruka kutoka eneo la tukio na kutua katika Barabara ya Kirwa baada ya bomu kulipuka.
Katika kila tukio hata kama ni hatari kwa kiasi gani lakini vibaka hawakosekani kama unavyowaona hawa wakiwa wamekamatwa na askasi wa polisi.
Askari wa Usalama Barabarani na Polisi wakiwa wametanda katika maeneo hayo ili kuangalia usalama wa watu na kuzuia watu kuenda eneo la Tukio.
Kamishna wa Oparesheni ya Polisi Paul Chagonja akiongea na vyombo mbalimbali vya kimataifa ikiwemo BBC na Dauch Welle.
Waandishi mbalimbali wakiwa kandokando ya njiapanda ya kwenda kambini huko hakuna anayeruhusiwa kuingia huko kwani hali bado si salama mpaka sasa na mabomu bado yanalipuka.
Eneo la Mbagala Zhakem mahala ambapo kuna barabara inayoingia katika kambi ya jeshi ambako Ghala la kuhifadhia Silaha lielipuka likiwa limezungushiwa uzio milipuko hiyo imeleta Kizaazaa kwa wakazi wa jiji la Dar es alaam na , hakuna mtu wala Mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kuingia katika eneo la tukio Vikosi vya jeshi la ulinzi, zimamoto na Polisi wote kwa pamoja wanajaribu kuzuia watu wasiende katika eneo la tukio.
0 comments:
Post a Comment