Waziri wa Nishati na Madini Mh. Wiliam Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo wakati alipotangaza kuufunga rasmi mjadala wa kuzungumzia ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans ili kuacha sheria na taratibu za manunuzi zifuatwe kama kutakuwa na haja ya kununua au lah, ameongeza kuwa kununua mitambo iliyotumika sia jambo geni jambo muhimu ni kufanya tathimini ya kitaalam kuhusu ubora wa miatmbo na utaratibu wa kisheria juu ya ununuzi wake hata hivyo Waziri Ngeleja hakuweka wazi kama Tanesco itanunua miatambo hiyo au haitainunua. kwa habari zaidi fuatilia vyombo mbalimbali vya habari kulia ni Naibu waziri wa wizara hiyo Adam Malima.
MJADALA WA UNUNUZI WA MITAMBO YA DOWANS UMEKWISHA!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment