Tanzania kwa mara nyingine tena imeshiriki kwenye maonyesho makubwa ya Utalii hivi karibuni yaliyofanyika katika jiji la New York yaloyojulikana kama "The New York time travel show".
Maonyesho haya yalishirikisha nchi nyingi na yalifanyika kwenye jumba kubwa linalojulikana kwa jina la Jacob Javids Senta wa zamani wa jiji hilo la New York.
Tanzania iliwakilishwa na maafisa mbalimbali kutoka Bodi ya Utalii TTB, Ngorongoro na makampuni binafsi yanayofanya kazi ya kuhudumia watalii, bodi ya utalii iliwakilishwa na Meneja masoko wa bodi hiyo Bw. Godfrey Meena wakati ngorongoro iliwakilshwa na C. Chikoti na E. Lomoyani, S Lelo na wawakilishi wa bodi hiyo ambao wako nchini Marekani (Bradford Group).
Kwa upande wa sekta binafsi wawakilishi walitoka makampuni mbalimbali kama vile Easy Travel Tours M. Carneiro, M Gullamhussein S. Hilji, Zara Tanzania Adventure M. Adam, V Maltman, kutoka kampuni ya Nunuri Safari Company iliwakilishwa na J. Malago.
Maonyesho hayo yalifanyika kuanzia tarehe 5-8 February 2009 ambapo marekani ni nchi ambayo imekuwa ikileta watalii kwa wingi nchini Tanzania kuanzia mwaka 2007 na ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa makampuni yanayoendesha biashara ya Utalii chini imeonyesha kuwa pamaoja ta matatizo ya kuanguka kwa uchumi katika soko la kimataifa ambayo yameikumba pia Marekani lakini watalii kutoka nchini humo wanaokuja nchini wameongezeka mara dufu na wanapenda zaidi kuja kutembelea utalii waTanzania hii ni habari njema jamani sana wadau FULLSHANGWE inaitakia mafanikoa mema Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja bodi ya Utalii nchini kwa mikakati yao ya kuboresha huduma za utalii nchini na kutangaza vivutio vilivyopo nchini tuko pamoja katika kufanikisha hilo.
0 comments:
Post a Comment