Meneja mkuu wa Pride Tanzania Bi. Shimimana Ntuyabaliwe akizungumza na ujumbe kutoka China uliotembelea katika shirika hilo tawi la Buguruni ili kujionea shughuli za shirika ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Pride Tanzania na kujadili mikakati ya kupunguza umasikini na kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizi mbili.
Mashine hizi zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kutotolea mayai kwa wenye kufuga kuku SIDO Dar es alaam ni mkombozi wenu tembeleeni huko.
Fundi mchundo Robert Samira akiyeyusha chuma kwa kutumia mashine yenye moto mkali ili kutengenezea vipuri vya magari vijulikanavyo kama U. BOLT kwenye shirika la viwanda vidogo SIDO jijini leo
Afisa Msaidizi wa mwenyekiti wa Pride Tanzania Mh. Idd Simba Bw. Mussa Mhando kulia akiwaongoza wageni mbalimbali walipotembelea katika shirika la viwanda vidogovidogo SIDO barabara ya Nyerere leo wageni hao walikuwa na semina ya siku mbili kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski iliyokuwa ikijadili upunguzaji wa umasikini kwa Tanzania na China na iliandaliwa na shirika la PRIDE Tanzania.
1 comments:
Siyo mbaya lakini kwa ushauri wangu jamani tujaribu kuwapatia vifaa vya kujilinda na ajali maana hapo moto wake si wakawaidana vilevile angalieni afya zao (HEALTH AND SAFETY)
Post a Comment