Mwanamuziki Joe Lewis Thomas kutoka Marekani leo jioni amelonga na waandishi wa habari mbalimbali katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, akizungumza na kujibu maswali Joe amesema amekuja nchini kufanya mambo makubwa katika onyesho lao litakalofanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders jijini kuanzia saa 1:00 jioni mpaka saa 7:00 usiku.
Joe Thomas atakayeshirikiana na wanamuziki wenzake kutoka kundi la Boyz 2 Men ambalo litawasili jijini kesho asubuhi, na wanamuziki wengine kutoka JamaicaTante Metro na Devonte Whos' ambao wanatarajia kufanya mambo makubwa jukwaani hapo kesho.
Joe Thomas ameulizwa maswali mengi na waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kwamba anaonaje Barack Obama kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani, Joe amejibu kuwa yeye mwenyewe alimpigia kura Barack Obama kwakuwa ni mtu ambaye anaonekana kuyafahamu vizuri matatizo ya wamarekani walio wengi na anaonekana ana nia ya kuifanyia mabadiliko Marekani
0 comments:
Post a Comment