Mgombea umakamu mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na mchezaji wa zamani wa Yanga Lawrence Mwalusako jana alikuwa ni mmoja wa wachezaji wa timu ya Tanzania Stars waliocheza na kuivurumisha bila huruma magoli 5-2 timu ya Union ya upanga katika mchezo mkali wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa taifa wa zamani jana asubuhi.
Timu ya Union upanga ndiyo ilianza kuifunga timu ya Tazania Stars katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakini kadiri muda ulivyosogea Tanzania Stars ilianza kulianda lango la Union kwa kasi na kuanza kurudisha goli moja baada ya lingine Lawrence mwalusako ambaye aliingia katika kipindi cha pili cha mchezo pamoja na Abubakary Kombo wakisaidiana na kocha wa Azam Fc Club, Syrivester Mashi waliuongezea kasi mchezo huo na kuifanya Tanzania Stars kuanza kupachika magoli kama wanavyotaka.
Mkocha wa timu hizo Kasongo Athuman wa Tanzania Stars na Mohamed Mmachinga walikuwa hawatulii katika viti vyao ili kuhakikisha kila timu inajipatia ushindi hata hivyo mpaka mwisho wa mchezo huo Tanzania stars ndiyo iliyotoka kifua mbele uwanjani kwa ushindi wa magoli hayo matano kwa mawili ya Union ya Upanga
0 comments:
Post a Comment