Shindano la aina yake la ubunifu linalodhaminiwa na Bia ya Reds linatarajiwa kufanyika katika Hotel ya Kilimanjaro Kempiski jijini ijumaa Oktoba 24 2008 ambapo shindano hilo ndiyo kitakuwa kilele Cha kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika mashindano makubwa kabisa Afrika ya ubunifu yatakayofanyika nchini Botswana.
akizungumza na waandishi wa habari meneja wa kinywaji cha Redd's George Kavishe amesema shindano hilo litajumuisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ili kutoa changamoto miongoni mwa wabunifu ili tupate mwakilishi bora katika ubunifu.
Katika shindano hilo burudani zitatolewa na mwanamuziki Banana Zoro na Bendi yake ya B. Band kwani tuna imani atatoa burudani murua kwa kuwa ana vibao vingi vikali kama vile "Nzela" ambacho kimekuwa kikitesa karibu nchi nzima kwa ubora wake.
Ameongeza kuwa pia kutafanyika Onyesho la mitindo litakalojumuisha wabunifu kama Farouk Abdela kutoka Zanzibar, atakayeonyesha mavazi yaliyopata jina la "Under the Veil" Masoud Kipanya, Monika kutoka Morogoro na Criss Designs wa Mwanza ambapo pia mlimbwende wa kimasai Neshno aliyeshiriki shindano la Face of Tanzania anayesoma na kufanya kazi wilayani karatu kwa sasa atashirika katika onyesho hilo, huku mmoja wa majaji akiwa Nsonwabile Ndamase toka Afrika kusini aliyejipatia umaarufu kwa kubuni shati maarufu la maua linalopendelewa kuvaliwa na mzee madiba (Nelson Mandela).
Mshindi wa Shindano hilo katika ubunifu ataiwakilisha nchi katika shindano la RAFDA la Afrika litakalofanyika Botswana, na tikaeti kwa ajili ya Fainali hizo zinazuzwa sh. 20.000 zinapatikana kwenye ofisi za Beautfull Tanzania Agency, Hugo House, Renzo Saloon mikocheni, Aqua Video Riblary, duka la Vitabu la Novel Idea, Shoppers Plaza, Mlimani City, Slipway Sea Cliefvillage, Steers na Samora Evenue.
0 comments:
Post a Comment