Injuries shatter Tanzanian marathoners´ dreams!!

Andrea Silvini running the marathon
Isegwe leading along with Dejene Yirdaw of Ethiopia

By Our Correspondent,
Berlin Tanzanian long distance runners, prospects of scooping top honours in the 42.km marathon race at the world championship was shattered by injuries that prevented Christopher Isegwe and Lucian Hombo from finishing the race over the weekend. Christopher Isegwe, who went to the front with the leading pack in the first 16km sustained a serious achilles tendon injury when the race hit 17km mark but struggled up to 27km when it became impossible to continue with the race. ``Despite some nagging pain at my achilles tendon I concentrated on maintaining a sustained and consistent speed but at 27 kilometre I had to succumb to the injury''. Lucian Hombo ran steadily up to 34 kilometres where he sustained a harmstring injury and dropped leaving Faustin Baha, Geturi Bayo and Andrea Silvini to finish the race. Among the over 110 elite runners, Faustin Baha was the first Tanzanian to hit the finish line in 2:17.11 to become 28th in a race that involved over 110 top long distance runners from all over the world. Getuli Bayo finished 57th in 2:25.52 earning his season best time while Andrea Silvini finished 60th in 2:28.48. The race was won by Kenyan Abel Kirui who finished in 2:06.54 setting his career record. “When I was reaching the finish line I still couldn’t believe it,” he said. “But I love running in Berlin. I know it so well from my times here with Haile Gebresellasie, and that made it so special for me. I love this city. When I got off the plane I knew then I could win, I was so confident. This morning I prayed with my coach for help, but I was so sure I would do it,” said Kirui after the race. Commenting about the results, the Assistant Secretary General for Athletics Tanzania, Julius Musomi said ``There is no witch-hunt, our runners were well prepared and in good spirits but we were not luck, because the weather was good, temperature was 18 degrees celsius and humidity was 73 per cent at start while it was 21 degrees celsius and 49 per cent humidity at finish``.

WAISLAMU NCHINI WATAKIWA KUACHA MAOVU!!

Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia akisalimiana na Waziri wa Kazi Ajira na Vijana katika moja ya matukio waliokuwa pamaoja.

Na Anna Nkinda - MaelezoDar-Es-Salaam
Waislamu nchini wametakiwa kutenda matendo yaliyo mema na kujiepusha na maovu katika maisha yao ili waweze kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya wakati akiongea na Waislamu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika viwanja vya Mnazi Mmmoja. Waziri Kapuya ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano hilo aliwataka waislamu hao pia kufuata nguzo tano za imani yao ambazo ni kutoa shahada, kusimamisha swala, kufunga mwezi wa Ramadhani, kutoa zaka na kwenda kuhiji Makka kwa wale wenye uwezo. "Watukufu Waislamu ninachosema hapa ni kwamba binadamu ameumbwa, ataishi, atakufa, atafufuka, atahukumiwa na baada ya hapo ataishi katika raha au mateso kutokana na vitendo vyake hapa Duniani hivyo basi ni wajibu wenu kuishi kadri ya neno la Mungu linavyosema", alisema. Akiongelea umuhimu wa kufunga wakati wa Mwezi wa Ramadhani Waziri Kapuya alisema kuwa kufunga ni amri na lazima kwa kila muislamu kama Mwenyezi Mungu anavyosema katika aya ya 183 ya Surat Al-Bakara.

KIVAZI CHA MDAU KUTOKA JAMBO LEO!

Huyu ni Mdau Said Mwishehe kutoka Gazeti Jambo Leo akiwa amepozi na kivazi chake cha leo, kilichotuvutia wana FULLSHANGWE mpaka tukamleta kwenye ukurasa huu lakini kilichotuvutia zaidi ni Kofia yake tu maana aah we acha tu.

TBC1 YATOA MAAFISA HABARI SIMBA NA YANGA!!

Cliford Ndimbo wa pili kutoka kushoto ambaye tayari amelamba dume kama afisa habari wa Timu ya Simba, Je vipi wanahabari wengine nao watatokaje? wa kwanza kushoto Baruan Muhuza,watatu Juma Nkamia, Evance Mhando na Enock Bwigane, picha hii ilipigwa tarehe 26/ March 2008 siku ya uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam.


Kulia aliezibwa na Camera ndie Louis Sendeu akiwa anava microphone akijianda kumuhoji mchezaji wa mpira wa Kikapu wa Kitanzania anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA Hasheem Thabeet kwenye kipindi cha kila wiki cha Michezo cha kwenye Luninga kinachoitwa MEZA YA MICHEZO kinachorushwa na Television ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayoitwa TBC1 hapo August 16/ 2009.Hii leo jumamosi 22 August 2009 baada ya kupita wiki moja Louis Sendeu ametangazwa na timu ya ligi kuu Tanzania bara ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA) kuwa msemaji wa timu hiyo ikiwa siku moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu mpya wa 2009 - 2010.Yanga ni miongoni mwa timu zilizochelewa kutimiza azimo la Bagamoyo la kila timu za ligi kuu Tanzania bara kuanzi msimu huu wa 2009 - 2010 kuwa na watendaji watu wa kuajiliwa.Mwingine alieula Yanga ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Yanga Lawrence Mwalusako ambae yeye amekuwa katibu mkuu na mtunza pesa ni Godfrey Mwenje.Sendeu anakuwa mwandishi na Mtangazaji wa pili toka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa msemaji wa timu ya ligi kuu wa kwanza alikuwa ni Cliford Ndimbo aliechukua cheo kama hicho kwenye timu ya Simba.Kila la heli mwanahabari mwenzetu Louis Sendeu katika ajira nyingine pamoja na Cliford Ndimbo.

BERNAD MWAKYEMBE NA RASHID MATUMLA KUTOANA MANUNDU KESHO DDC!!


Bonddia Amour Mzungu kg 86 kutoka Zanzibar kushoto na Kiza Kinene kg 90 kulia wakitambiana kabla ya mopambano wao kesho katikati ni promota wao Shomari Kimbau.

Shomari Kimbau katikati akiongea na wanahabarimleo kutangaza mpambano huo kulia ni Bernad Mwakyembe na kushoto ni Rashid Matumla Snake Man.


POWER BREAKFAST YAWAPA BURUDANI YA KUKATA NA SHOKA WADU!!

Watangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi Gerald Hando na Babra Hassan wakiongea kwa kuigiza mbele ya wageni waalikwa kama wanavyotangaza redioni, wakati wa tafrija ya kujipongeza iliyoandaliwa mahsusi kwa wadau mbalimbali wa kipindi hicho ilifanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick jijini ambapo kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki wa kundi la Blue3 kutoka Uganda, Marlow na wasanii wa kundi matata la THT kutoka jijini, hebu mdau ambaye hukuwepo pata matukio katika picha ili kujua wadau waliojimuvuzisha na kuvinjari katika Tafrija hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka sisi FULLSHANGWE kama kawaida yetu tulipenya na kuingia humo na mambo yalikuwa Mujaraarabu kabisa.
Nyota wetu wa kikapu Hasheem Thabeet katikati ambaye anacheza mpira wa kikapu nchini Marekani na marafiki zake hawakuwa nyuma kupata burudani wakati wa tafrija ya kujipongeza ya kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi na Redio Clouds ya jijini.
Mdau wa siku nyingi katika muziki ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa mwanamuziki Mr II kutoka Marekani Nurueli kati, Sara wanablog wa angaliabonngo.blogspot.com kul;ia na mdau Lugano

Hapa ni Pipi mwanamuziki wa THT,P. Funk Producer maarufu nchini Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchmark Production na mwandaaji wa Bongo Star Search na mwanamuziki Sara wakipozi kwa picha.
Biggy murugenzi wa maduka ya Biggy Respect kushoto akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa Benchmark Production Ritah Paulsen kati kwa mbaali anaonekana P. Funk akiteta na Pipi mwanamuziki wa THT, Biggy Respect ndiyo kampuni iliyowavalisha mavazi washiriki wote wa Bongo Star Search 2009.
Blue3 wakiwa kazini kwa sasa ni kundi linalosumbua sana katika ukanda huu wa afrika mashariki kutokana na utunzi wao matata na vibao vyao ambavyo vinakubakika sana kwa mashabiki wao.
Hapa Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Juhayna Kusaga akipata shangwe za Blue3 na marafiki zake wakati kundi hilo lilipokuwa likifanya mambo yake jukwaani.

Mbunifu wa mavazi Farha na dada Rehema wa I-View Photography anayefuatia na marafiki zao

Eh hata waheshimiwa walikuwepo ilikuwa si mchezo jamani wadau paty la kukata na shoka.

Kulia ni Martha Bangu Meneja Masoko TDL kulia Babra Hassan mtangazaji wa Clouds kipindi cha Power Breakfast ambacho ndiyo hasa kiliwakutanisha wadau mbalimbali pale Movenpick jana na mwisho ni Mpelwa menejamasoo TBL.

Hapa Kinje Mkurugenzi wa KiKis Tours Kulia Ritah Paulsen na Ado Frans anayemiriki Club ya Taboo nchini Africka Kusini nao wakavinjari maeneo ya Movenpick ili kupata burudani.

wadau Tumi Makani kulia Richard Shelukindo kati na Mdau Jesse anayemiliki Club Afrique huko Uingereza nao walikuwepo ili kujua yaliyojiri katika Tafrija hiyo ya PowerBreakfast.
Adam Mchomvu mtangazaji wa kipindi cha XXL sasa ameanza kushika Camera ya Video, naona labda anafanya mazoezi kabla ya Kituo cha televisheni cha mjengoni hakijaanza ili aweze kukamata Dimba la kupiga Picha hongera kaka hapa anaonekanaakimuelekeza kitu mtangazaji mwenzie Rommy J. hapo mjengoni wa kipindi cha The Blog
Mkurugenzi wa Maduka ya Big Respect na mbunifu wa mavazi maarufu kama Biggy akiwa katika picha ya mpamoja na mwanamuziki wa siku nyingi aliyekuwa akiimba katika bendi ya African Stars Jesca Charles Jesca anayeishi Falme za Kiarabu hivi sasa amerejea nyumbani kwa mapumziko.

Nyota wa Kikapu nchini Marekani anayecheza Ligi ya NBA katika timu ya Merphs Mtanzania Hasheem Thabeet kulia akiwa na Meneja matukio na Promosheni wa Serengeti Breweriers Bahati Singh.
Waigizaji maarufu nchini Kanumba na Aunt wakifanya vibweka mbele ya Camera ya Kamanda mshika Camera wa FULLSHANGWE hebu wacheki mdau.

Mwanamama wa Iringa ajishindia Tank la Mafuta!!

MKAZI wa Iringa Jennifer Mlawa mwenye namba ya sim (0655450288) leo amejishindia tank la mafuta katika droo inayoendeshwa na kampuni na New Habari iitwayo Bamba Mafuta.
Droo hiyo ambayo ilichezeshwa kwa mara ya kwanza jana ambapo mkazi mwingine kutoka mkoani, Gabriel Mwasaga (0719 403832)wa Mbeya alijishindia pia full tank.
Akizungumza katika droo hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Udhamini na Matukio wa kampuni ya New Habari (2006), Petter Mwendapole amesema droo hiyo itakuwa ikifanyika kila wiki.
“Leo tumepata washindi wawili kutokana na wiki iliyopita kutokuchezesha, washindi hawa watakabidhiwa zawadi zao huko huko walipo,” amesema.
Droo hiyo iliyochezwa katika ofisi za Selcom mjini Dar es Salaam ilishuhudiwa na msimamizi kutoka Shirika la Bahati na Nasibu Tanzania, Umudi Abdulhussein na Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori.
Ili kushinda bahati nasibu hiyo unatakiwa kutuma neno MAFUTA kwenda namba 15331. Promosheni hiyo itafanyika kwa muda wa miezi mitatu.
New Habari ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai, The African, Mtanzania Jumapili, Weekend African na Dimba Jumapili.

Nelson Mandela Bay ready for 2010!!


In the city's colourful promotional brochure, Nelson Mandela Bay/Port Elizabeth boasts of being the "best tourist destination" in South Africa. After a short tour around the city, it is not hard to see why such a bold claim has emblazoned across the booklet's front cover.
Situated in the Eastern Cape Province, where some of the country's most celebrated figures hail from, there are many compelling reasons why Nelson Mandela Bay/ Port Elizabeth should be an essential stop for tourists during next year's FIFA World Cup.
"We believe the Nelson Mandela Bay will be one of the biggest tourist attractions during the World Cup," Nelson Mandela Bay spokesperson, Roland Williams told FIFA.com. "Our goal is to market and position the city as a destination of choice far beyond 2010. We have worked very hard and one can see that our infrastructure is one of the best in the country."
The warm beaches, the wildlife, the breathtaking views and the natural vegetation on view as you drive through this vast province go towards making a trip to the south-eastern part of the country a must. The Eastern Cape is home to Nelson Mandela, an iconic figure in South Africa and throughout the world. It has also given birth to the likes of another former South African president, Thabo Mbeki, as well as Steve Biko, the architect of Black Consciousness in South Africa, Govan Mbeki, Oliver Tambo, Walter Sisulu and many others.
Nelson Mandela Bay/Port Elizabeth is also the birthplace of Blackburn Rovers and Bafana Bafana winger, Elrio van Heerden. Currently, the city does not have a top flight outfit following the sudden relegation of Bay United from the elite league last season. However, some of the country's major teams continue to use the city for matches.
Recently, Nelson Mandela Bay launched three Visitor Information Centres (VICs) to ensure tourists arriving in the city for the 2010 FIFA World Cup™ receive the best advice and information. The three centres are based at the Port Elizabeth Airport, the lighthouse facility at the Donkin Reserve and the Boardwalk Casino and Entertainment World. These one-stop shops will supply tourists with information on a wide range of services, including reservations, accommodation, tours, vehicle hire, entertainment, adventure and travel tips. Visitors to the centre will also be able to make use of user-friendly touch screens linked to central database of tourism products on offer and the advertisements of local businesses.
New StadiumTwo months after its completion, the state-of-the-art Nelson Mandela Bay Stadium has already passed two major tests in its quest to be ready for the FIFA World Cup.
The stadium achieved a milestone when it became the first newly-built South Africa 2010 venue to be completed - a full 12 months before the world's greatest showpiece descends on the African continent for the first time ever.
The Nelson Mandela Bay Stadium recently hosted two major events: the British Lions Tour and the country's biggest football encounter popularly known as the Soweto Derby between historical arch-rivals Orlando Pirates and Kaizer Chiefs.
"It is clear for everyone to see that the Nelson Mandela Bay is ready," Williams added. "We managed to complete our stadium more than a year before the event; that on its own should say something to those who still believe we won't be able to successfully host this event."
The Nelson Mandela Bay Stadium will host group games during the 64-match event next year. The stadium will also be the venue for the third and fourth place play-offs By http://www.fifa.com/ .

KONGAMANO LA KUJADILI ATHARI ZA UANDIKISHWAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA PEMBA LAENDELEA JIJINI!!

Wanasiasa Mashuhuri nchini wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano mara baada ya mapumziko mafupi katika kongamano la kujadili Athari za Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Kisiwani Pemba linalofanyika leo pale Karimjee Hall, viongozi na wadau mabalimabli wa siasa wakiwemo wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanahudhuria Kongamano hilo, ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa wajumbe na kujadiliwa katika kongamano hilo na kutolewa mapendekezo ya hatua zitakazochukuliwa , kutoka kulia ni Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba, Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ,Katibu mkuu wa Zamani wa AU amabyo zamani ilijulikana kama OAU Salim A. Salim na Mwenyekiti wa Chama hicho Prf. Ibrahim Lipumba.

NAIBU WAZIRI KIONGOZI WA (SMZ) ALLY J.SHAMHUNA ATEMBELEA TSN!!

Naibu Waziri Kiongozi wa Saerikali ya Mapinduzi Zanzibar na waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Ally Juma Shamhuna akitoka katika ofisi za TSN mtaa wa Samora baada ya kutembelea Ofisi Hizo tayari kwa kuendelea na Ziara yake ambapo, alienda kutembelea mtambo wa kuchapia magazeti wa shirika hilo uliopo maeneo ya Tazara Jijini Dar es salaam, gazeti la DailyNews ndiyo gazeti kongwe kuliko yote nchini ambapo lilianzishwa mwaka 1972 na kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa mgeni huyo na uongozi wa TSN DailyNews ndiyo gazeti linaloongoza kwa mauzo hapa nchini kwa upande magazeti ya kiingereza.
Naibu WaZiri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ally Juma Shamhuna akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili katika ofisi za magazeti ya Serikali TSN leo asubuhi kwa ziara fupi kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kulia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Muungano Dr. Florens Turuka.

Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh. Ally Juma Shamhuna akitoka mara baada ya kutembelea ofisi za Magazeti ya Serikali TSN leo asubuhi.


Mtanzania Teddy Kalonga kwa mara nyingine tena anabeba bendera yetu, tumpigie kura!!


Mtanzania Teddy Kalonga kwa mara nyingine tena anabeba bendera yetu ughaibuni na hivi sasa amekuwa ni mmoja wa warembo wanaowania nafasi ya kuwa mtangazaji Luninga ya SPIKE TV.
SPIKE TV ni channel ya Michezo ya wanaume huko Marekani.
Teddy anatakiwa kupigiwa kura ili ashinde nafasi hiyo ambayo mwenyewe anasema hajawahi kuifanya maishani na anafurahi akiipata na kuahidi kulitangaza vyema jina la Tanzania.

“well, nilienda kufanya interview sikujua kama kutakuwa na mambo ya picha au competitions, ila ndio hivyo nimekuwa mmoja wa washindani” alisema Teddy alipoongea na Spoti Starehe leo. aidha nilimuuliza Teddy kama Channel hiyo inahusika na mambo gani ni michezo tuu ama naye alisema”…mambo mengi kama the most shocking reality things, cars, I mean vitu vingi vinavyopendwa na wanaume mostly”.
Piga kura yako hapa http://www.spike.com/spike-girl/500960

SAMSUNG YAIMWAGIA VODACOM MISS TANZANIA DOLA ZA KIMAREKANI 55.000!

Mkurugenzi wa Kampuni ya Smsung Patricia King'ori akionyesha moja ya simu zinazotengenezwa na Kampuni hiyo ambazo warembo watakaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania watazawadiwa Kampuni ya Samsung imeingia mkataba wa kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa Dola za Kimarekani 55.000 na itawapatia warembo wote watakaoshiriki shindano hilo simu aina ya (Samsung Star), wengine waliopo katika picha ni Hashim Lundenga mkurugenzi Miss Tanzania katikati na mwisho ni George Rwehumbiza Meneja Udhamini na Mawasiliano Vodacom Tanzania, hafla ya kutangaza udhamini hulo imefanyika leo Savvanah Lounge katika Hoteli ya City Paradise jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Samsung Patricia King'ori akimkabidhi simu aina ya Samsung Star mmoja wa warembo walioshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka jana Frolence Josephat wakati kampuni hiyo ilipotangazwa kuwa mdhamini mwenza wa Miss Tanzania mwaka huu kulia ni Ramesh Shah Jaji mkuu Miss Tanzania na kushoto ni Hashim Lundenga Mkurugenzi Miss Tanzania.

TAMASHA LA MICHEZO YA JADI KUFANYIKA MWISHONI MWA MAKA HUU!!

Mwenyekiti wa chama cha michezo ya jadi Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe akionyesha tuzo ya heshima ambayo chama hicho kilitunukiwa wakati kiliposhiriki katika tamasha la michezo ya jadi lililofanyika nchini Korea mwaka jana Tanzania ni nchi pekee iliyopata tuzo hiyo kati ya nci 30 zilizoshiriki katikatamasha hilo kutoka Africa, Mzee Mohamed ameonyesha tuzo hiyo wakati alipoongea na wanahabari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akielezea maandalizi ya michezo ya jadi ianayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwishoni ama mwezi wa kumina moja mwanzoni mwaka huu jijini Dar es alaam.

MHESHIMIWA DR OMARY MZERU NIBUKA KUWA MGENI RASMI MISS EAST AFRICA MOROGORO IJUMAA!!

Annete John Mshindi wa pili Miss East Africa mwaka jana akipokea mfano wa cheki kama kama malipo ya zawadi yaeke.

Mbunge wa Morogoro Mjini Dr . Omari Mzeru Nibuka ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye shindano la Miss East Africa Morogoro ambalo limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Masuka Village mjini humo. Wasichana wanaoshiriki shindano hilo ni Zaima Aman , Joyce Adam, Sharbano A Hamidu, Sofhia Waziri Mapepe , Neema Stanley, Herieth Andrew , Matlida J. Gille na Megy S . Nellson. Washiriki wengine ni Fatma Bonge , Farashuli Abduly , Mary Ladslaus na Rehema Said.Wadhamini wa shindano hilo ambao hadi sasa wamejitokeza ni Kiu Investment LTD , Iddi Baka Pandisha Fitness Centre , Screen Master na J.R.T Films Productions .Wengine ni Kakamie , Datastar Training College , K-P Wear , The Club , Vam General Supply Co ltd, The Premium Institute of Hotel Management, Morogoro Institute of Hotel Catering & Bussiness Management ,KP-Wear, The Klub, mtandao wa www.king kif.blogspot.com na http://www.ashabaraka.blogspot.com/.Kiingilio ni shilingi elfu tano (5000) kwa viti vya kawaida na shilingi elfu kumi(VIP) huku Afande Sele na ' jeshi ' lake wakifanya makamuzi ya ki-Hip-Hop kwenye jukwaa na baada ya shoo hii Afande Sele na ' jeshi ' lake wanatimka Ufaransa.

EVANCE MHANDO WA TBC1 AKIZUNGUMZA NA HASHEEM THABEET.

Mchezaji mpira wa kikapu wa Kitanzania Hasheem Thabeet anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA katika timu ya MEMPHIS GRIZZLES ya Tenesse akihojiwa na mwandishi na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Evance Mhando.
Mahojiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za TBC1 Mikocheni Jijini Dar es salaam siku ya jumapili August 16/ 2009 saa nane mchana ambapo Hasheem alienda kutembelea ofisi hizo na kushiriki kwenye kipindi cha wiki cha Michezo kinachoitwa Michezo Yetu kilichoendeshwa na Evance Mhando (Mr Names).
Pamoja na yote Hasheem aliwataka vijana wa Kitanzania kujitahidi kwenye michezo pia na kutilia mkazo suala la Elimu na kutokata tamaa mapema kwenye kila jambo wanalolitaka katika Maisha yao.

HUENDA NI KANISA JIPYA LIMEANZISHWA GYMKANA!!

Mdau Mac Temba ametumuvuzishia hii kali kama unavyoona katika picha Hawa ni waumini wa kanisa ambalo bado halijajulikana hapa walikutwa wakisali, wakiomba na kuimba nyimbo za kuabudu katika viwanja vya gymkhana mdau Temba ameomba na sisi tuimuvuzishe kwenu wadau anaomba kuwakilisha kwenu.