J&L HAND CRAFT YAFANYA KWELI KATIKA SOKO LA KIMATAIFA


Peremina Alfred Maagi wa kampuni ya J&L Hand Craft ya jijini inayojihusisha na kutengeneza mishumaa ya aina mbalimbali akiwa katika banda lake lililoko kwenye banda kuu la Benki ya NMB, Peremina amesema wana kiwanda maeneo ya Sinza Mori na duka lao liko Mbezi kwa Komba, Peremina ameongeza kuwa wana masoko mbalimbali nje na ndani ya nchi kwa mfano hapa nyumbani wanasambaza sehemu mbalimbali kwa watu binafsi, Mahotelini, kwenye misiba na makanisani ambapo katika masoko ya nje wanasambaza katika nchi za Ulaya na Asia kama vile Uingereza, Norway na Malaysia.

Ameongea kuwa wanaishukuru Benki ya NMB ambayo inawawezesha na kuwapa mkopo kwa wakati kila wanapohitaji ili kuendeleza mtaji wao,kampuni hiyo ilianza na mkopo wa
shilingi 1,000,000/= mpaka sasa wamefikia mkopo wa shilingi 3,000,000/= na wameendelea vizuri na biashara yao bila matatizo
Kwa mawasiliano zaidi kama unahitaji mishumaa kutoka J&L Hand Craft wasiliana nao kwa namba hizi 0754-280469/0784280469/0787-907292/0754426795 Email ni jlhandcraft@yahoo.co.uk


Dada Peremina Arfred Maagi kutoka kampuni ya J&L Hand Craft Dar es alaam inayojihusisha na utengenezaji wa mishumaa ya aina mbalimbali akitoa maelezo kwa mteja aliyemtembelea katika banda lake lililoko kwenye banda la Benki ya NMB katika viwanja vya maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu J.K Nyerere barabaraya Kirwa jijini Dar

VODACOM TANZANIA WAENDELEA KUSAJIRI NAMBA ZA SIMU!!


Wateja mbalimbali wakampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wameendelea kusajiri namba zao za simu katika banda la kampuni hiyo kwenye viwanja vya maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kirwa,ikiwa ni kuitikia agizo la serikali iliyoagiza kila kampuni ya simu za mkononi ihakikishe inazisajiri namba za simu za wateja wao ikiwa ni juhudi za kudhibiti mitandao hiyo kutumika isivyo halali.

Kikundi cha burudani kikitoa burudani kwa wateja waliotembelea kwenye banda la kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania katika viwanja vya maonyesho vya mwalimu J.K Nyerereyanayoendelea barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam.

HATIMAYE NYUMBU WAFANYA KWELI HEBU CHEKI HILI ROLI!!


Tuna kila sababu ya kulipongeza Jeshi letu la wananchi JWTZ hasa Kiwanda cha NYUMBU kwa kutengeneza Roli aina ya NYUMBU linalovutia hata kwa kulitazama na ambalo nadhani pia ni Imara sana, hii kwa kweli ni hatua kubwa najua tumetoka mbali sana na nimekuwa nahudhuria maonyesho mengi yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Barabara ya Kirwa kila mwaka, nimekuwa nikijionea Teknolojia ya NYUMBU inavyokuwa kila mwaka, kitu kinachonipa Matumaini na Faraja kubwa kwa upande wa Teknolojia yetu hasa katika kutengeneza Magari ipo siku tutaqkuwa mbali sana, Nilipopata maelezo katika banda hilo niliridhika na nikiona iko sababu ya Serikali yetu Kukiunga mkono kiwanda hiki ili kiendelee kufanya mambo mengine makubwa zaidi, sisi FULLSHANGWE tunawatakia kila mafanikiona tunajisikia fahari kwa kuwa na kiwanda kam NYUMBU na tunadhani kama kitaungwa mkono na Serikali yetu kwa kukiwezesha Fedha, Mitambo na mafunzo ya wataalamu kinaweza kuwa mkombozi wa Taifa hili kwa siku za usoni Hongereni sana NYUMBU.

SIMBA YALAMBA VIROBA VITATU VYA SUKARI YA MTIBWA LEO UWANJA WA TAIFA!!


Wachezaji wa Mtibwa Sukari wakijaribu kuzuia washambuliaji wa timu ya Simba wasiigie golini mwao wakati timu hizo zilipocheza kwenye uwanja wa taifa leo jioni ambapo simba imefanikiwa kuifunga mtibwa magoli matatu kwa moja huku timu hizo zikionyesha kiwango cha hali ya juu kisoka hali ambayo mashabiki wengi wameielezea kuwa ilichangiwa na waamuzi kutoka shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA ambao ndiyo waliochezesha waliochezesha mchezo huo, waamuzi hao wapo nchini ikiwa ni mpango wa FIFA katika kutoa mafunzo kwa waamuzi wetu hapa nchini nadhani waamuzi wetu watakuwa wamejifunza vyakutosha kama mafunzo hayo yalikuwa yakiingia vilivyo vichwani mwao lakini kama sivyo basi FIFA watakuwa wametwanga maji kwenye kinu.

Kikosi Cha Timu ya Mtibwa Sukari wana tamtam katika picha ya pamoja.

Kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba Sports Club katika picha ya pamoja.

Serikali yasaini mpango wa upatikanaji wa dawa za kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu nchini!!


Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Blandina Nyoni akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Mwanaidi Maajar katika moja ya shughuli zake za kitaifa.
Na Anna Nkinda – Maelezo

04/07/2009 Serikali imesaini muendelezo wa makubaliano ya miaka minne ijayo na Mfuko wa Maendeleo Endelevu wa Novartis AG wa Switzerland kwa ajili ya kutoa dawa za kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu nchini.
Makubaliano hayo ambayo ni ya kuanzia mwaka 2009 hadi 2012 yalifanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Blandina Nyoni na Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa Novartis AG Daniel Vasella na kushuhudiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika makubaliano hayo Mfuko wa Novartis AG watatoa dawa za kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu kwa wagonjwa wapya 250,000 kupitia Mfuko wa Dunia wa Kuhudumia Dawa (The Global Drug Facility - GDF) wa Shirika la Afya Duniani.
Mfuko wa Novartis AG unafanya kazi mbalimbali za afya hapa nchini tangu mwaka 1957 chini ya mwanzilishi wake Profesa Rudolf Geigy ambao ndio waanzilishi wa kituo cha utafiti wa maralia kilichopo Ifakara mjini Morogoro.
Aidha mfuko huo pia umekuwa ikitoa dawa kwa gharama naafuu chini ya Mpango wa Accredited Drug Dispensing Outlets (ADDO) ambao unaimarisha usawa wa upatikanaji wa dawa za maralia hapa nchini. Pia ni wasambazaji wa dawa mseto za maralia za ALU na kwa mwaka 2008 walitoa dozi 15.8 milioni.

BEATRICE LUKINDO KUTOKA IFM ANYAKUA TAJI LA WASOMI (MISS HIGHERLEARNING)


Miss Higherlearning 2009 Beatrice Lukindo akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Dorris Deonatus Kulia na mshindi wa tatu Esther Gao mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano la kanda ya Elimu ya juu lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es alaam

Hii ndiyo tano bora ya miss Higherlearning kutoka kulia ni Esther Gao,Dorris Deonatus, Beatrice Lukindo na Linda Mzinga mara baada ya kutangazwa kwa warenbo walioingia tano bora ya shindano hilo.

Mkurugenzi wa Ubunifu wa kampuni ya kubuni mitindo ya mavazi ya CarpuanyDesign Grace Sinamtwa kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Mathew Lauwo katika shindano la kumsaka mrembo wa elimu ya juu kwenye ukumbi wa Karimjee usiku wa kuamkia leo kampuni hiyo pia ilidhamini shindano hilo.

Huyu ndiyo yule Rapa machachari wa bendi ya Africa Stars anayekwenda kwa jina la "Furgasony" akighani kwa mbwembwe huku akipelekwa puta na mmoja wa wanenguaji wa kundi hilo.

Wanengaji wa bendi ya African Stars walifanya mambo makubwa katika onyesho hilo kama unavyoona wakiwajibika jukwaani.

Waimbaji wa kundi maarufu la African Stars wana wa kutwanga na Kupepeta wakiimba kwa hisia katika onyesho la Miss Higherlearning lililofanyika kwenye ukumbi wa karimjee usiku wa kuamkia leo ambapo mrembo Beatrice Lukindo ameibuka kidedea na kuwakilisha kanda ya wasomi katika shindano la Vodacom Miss Tanzania hapo baadae mwaka huu.

Mdau Edwin Temba akiwa na mdogo wake Innocent Minja.

Afisa Bidhaa wa Vodacom Elihuruma Ngowi kushoto akiwa na Meneja Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna katika shindano hilo wakifuatilia kwa karibu kila kilichoendelea.

Afisa Habari wa Vodacom Matina Nkurlu awa mpiga picha hebu mcheki anavyohangaika na Camera hapa akitafuta tukio lililomvutia wakati wa shindano la Miss Higherlearning kwenye ukumbi wa Karimjee usiku wa kuamia leo.

COME AND REGISTER NOW AT ALLIANCE FRANCAISE

Learn at your pace:
? Choose between extensive, semi-intensive or intensive classes
? Come for classes once, twice, three or four times a week.

Course Prices for 2009
Cost per session of 10 weeks
Children and teens
Saturday morning for children (2 hrs once a week) 80,000 Tsh
Text books and activity books:
Grenadine 1, Grenadine 2 45,000 Tsh
Saturday afternoon for teenagers (2 hrs once a week) 80,000 Tsh
Text books: Kiosque 1, Kiosque 2 35,000 Tsh

Adults
Conversation (2 hrs once a week) 60,000 Tsh
Day time (2 hrs twice a week) 85,000 Tsh
Saturday (4 hrs once a week) 95,000 Tsh
Evening (2 hrs twice a week) 95,000 Tsh
Early morning (1.30 hrs three times a week) 95,000 Tsh
Evening semi-intensive (2 hrs four times a week) 190,000 Tsh
Text books: Taxi 1, Taxi 2, Taxi 3 35,000 Tsh
Children Holiday intensive (2 weeks in July) 250,000 Tsh

Private classes from 25,000 Tsh
On-site Business French Tuitions: contact AF

New intensive Kids courses !

Holiday intensive classes !
Specifically designed for primary school students (Grade 3-4-5)
Lots of recreational activities planned.
Have fun and learn French at the same time is another way to
optimize your kids school holidays. 12 students max. per class
Venue: French School (Oysterbay)


More info :
*******
Julie / Pascal:
Tel : +255 (22) 2131 406
Mobile AF: 0755 481 374
E-mail : courses@afdar.com
www.ambafrance-tz.org

UKITAKA KUTOKA KIBRINGBRING NA PAMBA ZILIZOENDA SHULE NENDA CLASSIC WEAR!!


Nguo mpya zimeingia sokoni katika Duka la Classic Wear Ukitaka kutoka Briingbriing kwa viwalo babkubwa kwa upande wa wanaume, wanawake na watoto nenda Classic Wear Duka kubwa la nguo za kila aina lililopo Vertenary Oilcom Petrol Station Tazara katika Barabara ya Mandela utapata kila unachohitaji kwa mavazi ya aina zote na Vipodozi kwa mawasiliano zaidi piga simu No 255773-666080 au 255717-607000 Email abubakar110@hotmail.com









TANZANIA DISTILLERIES LTD NA MAMBO MAKUBWA SABASABA!!


Meneja masokowa Tanzania Distilleries Ltd Martha Bangu akiwaelekeza kitu wafanayakazi wa kampuni hiyo katika banda lao kwenye maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere barabaraya Kirwa jijini Dar, maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi leo na Rais wa Malawi Mh. Bingu wa Mutharika kampuni hiyo inazalisha vinywaji mbalimbali kama vile Konyagi, Savanna, Overmeer, Valeur,Amarula na vingine vingi wakazi wa jiji tembeleeni banda hilo na kujionea mambo mbalimbali kutoka kampuni hiyo.



Mfanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd Bw. Mnyonge Mnyongeni akiwahudumia wateja waliotembelea katika banda la kampuni hiyo kwenye maonesha ya 33 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea hivi sasa kwenye viwanja vya mwalimu J. K. Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam.

DYNAMIC YOUTH CHANNEL KIDSCO LAUNCHES ON DStv!!



June 2009

From Tuesday June 30, DStv audiences in East and Central Africa* will have access to the dynamic youth channel KidsCo when it’s added to the DStv Premium, Compact and Family bouquets.

KidsCo, the international children's channel owned by leading media companies NBC Universal, Cookie Jar Group and Corus Entertainment Inc., has also secured an agreement with MultiChoice Africa for KidsCo to air in 13 countries in Africa on the DStv platform. KidsCo will be available in 11 countries via satellite in English and in Mozambique and Angola in Portuguese and will also be available on cable pay TV.

Commenting on the new channel offering Eben Greyling (President: MultiChoice Africa) said, "We are happy to offer the channel to our subscribers as it adds great value to our existing bouquets by enhancing the entertainment experience for the whole family."

Children and families in Africa can look forward to wholesome and age appropriate programming from KidsCo, including The Wiggles, Inspector Gadget, New Adventures of Madeline, Sabrina, Tracy Beaker, Dennis the Menace and original KidsCo programming including arts show, Jass Time! and KidsCo's recently commissioned environmental series for 6-10 year olds, Boo & Me.

Paul Robinson (KidsCo Managing Director) commented: "We are extremely pleased to be working with MultiChoice and look forward to partnering with them in building the KidsCo brand in Africa. KidsCo's presence in Africa has grown rapidly and we are delighted to be able to offer KidsCo's particular brand of fun and learning-based programming to African families."

KidsCo is the home of entertaining and educational programming. A fun, but safe environment for children, it's a TV adventure playground interacting with audiences of all ages, 24 hours a day and 7 days a week. Offering three programming zones of preschool, kids 6-10 and family, KidsCo has been designed to fit audience availability and lifestyle, and features great animated and live action content plus movies which can be enjoyed by the whole family. Viewers around the world have already embraced KidsCo and recognise how it connects families by providing safe, trusted, age-appropriate and educational programming to kids everywhere.

*Available in Angola, Burundi ,Central African Republic, Congo, DRC, Equatorial Guinea, Gabon, Kenya, Mozambique, Rwanda, Tanzania, Uganda and Zambia.

KAMPUNI MPYA YA SIMU ZA MKONONI SASATEL KUMKOMBOA MNYONGE KATIKA MAWASILIANO!!

Mfanyakazi wa Kampuni mpya ya Simu za mkononi Sasatel bw. Kayitana akiwaelezea wakazi wa jiji la kampuni hiyo katika maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa Sabasaba, jinsi mtandao wa kompyuta wa kampuni ya Sasatel unavyofanya kazi ya mawasiliano kwa Internet na jinsi mtandao huo unavyoweza kurahisisha mawasiliano kwa wateja wake

Wafanyakazi wa kampuni mpya ya simu za mkononi ya Sasatel wakijadiliana jambo katika banda lao kwenye maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa Sabasaba katika viwanja vya mwalimu J. K. Nyerere Barabara ya Kirwa maonyesho hayo yatafungiliwa rasmi kesho na Rais wa Malawi Mh. Bingu wa Mutaharika na yataendelea mpaka tarehe 10 julai.

Wakazi wa jiji wakiangalia kikundi cha burudani cha Worrias Academia cha Mwananyamala wakati kilipokuwa kikitumbuiza kwenye banda la kampuni mpya ya simu ya Sasatel ya jijini katika maonyesho ya 33 ya Biashara ya kimataifa Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu J. K. Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam.

AT ALLIANCE IN JULY!!

MaKuYa exhibition:Opening: Friday 10 July, 6.30pm, FREE!Open from 11 to Sat. 25 July, Mon. to Sat., 10am-6pmExhibition Hall.“ A window into the traditional performing and cultural arts of southern Tanzania”The exhibition will be also showcasing the work of ADEA (The African Development Align CenterthoughEconomic and Arts) in Mtwara, from 14 to 16 August 2009 for the second edition of the MakuyaFestival.The aim is to preserve, promote and perpetuate the traditional culture and performing artsof Makonde, Makua and Yao tribes in the region through the MaKuYa Festival.The purpose is also to catch the audience attention through exhibition to understand thehistory and the uses of Masks in dances.Photograph and Traditional clothes will also be exhibited.The exhibition is organized by Alliance Française in partnership with MaKuYa Festival andThe centre for African Development through Economic and the Arts.Contact Alliance : Cultural coordinator :Tel : +255 (22) 2131 406Mobile AF: 0755 481 374E-mail : cultural@afdar.com

Kwaya ya The Boys Choir of Kenya yafanya kweli ndani ya Studio za BBC!!

Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilitembelewa na kundi la kwaya ya vijana kutoka Kenya, The Boys Choir of Kenya, ambapo pamoja na mambo mengine walitumbuiza kwa nyimbo kadhaa. Kwa kifupi katika studio hizo hivi ndivyo ilivyokuwa.Ndani ya mojawapo ya studio za matangazo ya BBC, vijana waliungurumisha mawimbi kwa vibao mbali mbali ikiwemo Hakuna Matata habari kwa hisani ya Tivuti (BBC SWAHILI.com).

MDAU MAC TEMBA ANA SWALI KUHUSU HII PICHA!!

"Kaka huyu albino wa hapa salenda kwanini anaomba wakati ana uwezo na nguvu ya kufanya kazi.wadau mnasemaje?
Hii picha nimempiga leo asubuhi akiwa anaomba pale salenda"
Hii picha imetumwa kwetu na Mdau Mac Temba juu ya kijana huyu Albino ambaye anafanya shughuli za kuomba kwa wapita njia wanaopita na magari yao pale makutano ya barabara Salenda na ile inayoelekea Kinondoni, ukizingatia kwamba walemavu wa ngozi wana tatizo la kuona pia kitu ambacho kinahatarisha maisha yake kutokana na magari mengine kwenda kwa kasi

WASANII WA TANZANIA WAENDA ALGERIA KUHUDHURIA TAMASHA LA PAN AFRICAN FESTIVAL!!

Mh. Balozi wa Algeria Nchini E Abdelmoun’aam, akiwa amembeba mtoto Coletha Benedicta huku wasanii wengine wakifurahia wakati walipofanya Tafrija na kuagwa katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo Upanga Takriban wasanii 52 na maofisa wa serikali 10 wameondoka leo kwenda nchini Algeria kushiriki katika Tamasha la Pan African Festival linaloanza Jumapili julai 5 mpaka julai 20 nchini humo FULLSHANGWE tunawatakia kila mafanikio watanzania wote wanaokwenda nchini humo kuiwakilisha nchi yetu.
Wasanii wawili ambao ni watoto lakini wana uwezo mkubwa kucheza sarakasi wa kundi la Splendid Thietre Group kutoka Ilala Coletha Benedicta kushoto na Vailet Saston ni miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania wanaotarajiwa kutisha katika tamasha la Pan Africa Festival litakalofanyika nchini Algeria kuanzia Julai 5 mpaka 20 mwaka mwaka huu wasanii hao wameondoka leo na ndege kutoka shirika la ndege la Algeria.
Kundi la ngoma za Asili la Bota kutoka kijiji cha Mtakuja Tarafa ya Lulindi Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakipozi kwa picha nje ya Ubalozi wa Algeria tayari kwa safari yao kwenda kushiriki Tamasha la Pan African Festival litakalofanyika kuanzia julai 5 mpaka julai 20 jijini Algeris jumla ya wasanii tofauti 52 wakiongozana na maofisa wa serikali 10 wanaondoka leo kwenda nchini humo kwa ajili ya tamasha hilo.


WAANDAAJI MISS HIGHERLEARNING WATANGAZA ZAWADI!!

Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akisisitiza jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari na waandaaji wa Miss Higherlearning leo uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Lundenga amsifu juhudi zilizofantwa na Kanda ya Vyuo vikuu katika kuboresha shindano hilo ukilinganisha na kipinfdi kilichopita kushoto ni jumbe wa Kamati ya maandalizi miss Higherlearning Zabron Mangare.
Mwanamuziki wa bendi ya African Stars Lwiza Mbutu akiimba kibwagizo cha wimbo wa Bendi hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari na waandaaji wa Miss Higherlearning kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo ambapo bendi hiyo itatoa burudani katika shindano hilo litakalofanyika ijumaa julai 3 kwenye ukumbi wa Karimjee, kulia ni mkurugenzi wa Manka Mushi Promotion Manka Mushi.

Kampuni ya Manka Mushi Promotion inayoandaa shindano la Miss Higherlearning imetangaza zawadi za washindi watakaoibuka katikashindano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee julai 3 ijumaamwishoni mwa wiki hii, ambapo zawadi zimeboreshwa kwa kiwango cha juuhivyo itawafanya washindi wajisikie wamepata kitu kizuri, pamoja nakwamba lengo la shindano hilo ni kuwapata washiriki watakaoletaushindani katika shindano kuu la Vodacom Miss Tanzania hapo baadae.
Zawadi hizo zimepangwa katika viwango vifuatavyo ambapo malkia washindano hilo atanyakua Fanicha zenye thamani ya shilingi m. 1.500.000na fedha taslimu shilingi 500.000, Mshindi wa pili atajipatia fanichazenye thamani ya shilingi m. 1.000.000 na fedha taslimu shilingi350.000, mshindi wa tatu atapata Fanicha zenye thamani ya shilingi500.000 na fedha taslimu shilingi 250.000, Mshindi wa nne atafanyashoping katika duka la nguo la Zizzou Fashion yenye thamani yashilingi 150.000 na fedha taslimu shilingi 200.000 na wa tano atapatashilingi 100,000 na zawadi kutoka duka la nguo la City Star Boutiquewakati washiriki wengine watapata kifuta jasho cha shilingi 50.000kila mmoja.
Warembo watakaopanda jukwaani ni 12 ambao ni Mwantumu Yasuph, BeatriceKinyto, Linda Mzinga, Magreth Beatus, Dories Deonatus, Jenny Rapoo,Easther Gao, Frabcisca Mansilo, Beatrice Lukindo, Aisha Ricoh naVeronica Mick, warembo hao wako kambini katika Hoteli ya Giraffe OceanView iliyoko Mbezi Beach katika ufukwe wa bahari ya hindi wakijifuakwa ajili ya kinyang’anyiri hicho ambacho kitapewa Burudani ya kukatana shoka kutoka Bendi ya African Stars na kikundi cha burudani kutokaAsia International Youth Felloship huku kiingilio kikiwa viti maalum 20.000 na kawaida 10.000
Shindano hilo linadhaminiwa na makampuni mbalimbali kama vile Vodacom,TDL – Submiller, Ben Expedition Tours, Air Tanzania, Ndege InsuranceCo,.Tesco Furniture, Clouds FM , Leo tena, Perfect Solutions, GlobalPublishers, Billcanas, Rozella Saloon Fullshanwe.blogspo, City StarsBoutique, Dollywood, Varley Spring, Girafe Ocean View Hotel , AuroraSecurity, Carpuany Design, Hattman Production, Paka Wear, na MustafaHassanali.