WAKUU WA SHIRIKA LA BIMA WAKUTANA NA MAMENEJA WA SHIRIKA HILO UBUNGO PLAZA!!

Mkurugenzi wa Shirika la Bima Bw. JustinE Mwandu akiongea na mameneja wa shirika hilo kutoka matawi ya mikoa mbalimbali nchini katika mkutano unaokutanisha watendaji wa shirika hilo kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza jinini Dar es salaam.

Mkurugenzi huyo amesema mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo kufahamiana na kupanga mikakati mipya baada ya shirika hilo kuundwa upya na kutoa ajira mpya kwa watendaji wake juu ya mambo kadhaa ya kutilia mkazo ili kusonga mbele kutendaji na katika huduma kwa wateja wa shirika hilo.

Mkutano umejumuisha mameneja kutoka mikoa 24 ya Tanzania, mameneja wa makao makuu na vitengo vya masoko kwa bima ya za maisha, Bima zisizo za Maisha na Utawala na Fedha.
Mwnyekiti wa Bodi wa Shirika la Bima la Taifa NIC kulia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Aloyce Mwasuka wakimsikiliza mkurugenzi wa Shirika hilo Justin Mwandu wakati alipokuwa akiwasilisha mada yake kwenye mkutano huo wa siku mbili unaohusisha mameneja wa Mikoa na vitengo mbalimbali katika shirika hilo.
Picha zikionyesha wajumbe mbalimbali waliohudhuria kwenye mkutano huo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika hilo Justin Mwandu.

wakiwa katika picha ya pamoja.





Meneja masoko Henry Machoke kulia na Mkuu wa mahusiano Mwanaidi Shemweta.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment