WAKUU WA NCHI NA MKUTANO WA JUKWAA LA UCHUMI WA DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM!!


Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro wakifatilia mada kwenye mkutano wa jukwaa la kujadili uchumi wa dunia kwa Afrika unaondelea Jijini Dar-Es-Salaam.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)
Dk. Batlida Burian akizungumza na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano wakati wa mkutano wa jukwaa la kujadili uchumi wa dunia kwa afrika unaoendelea Jijini Dar-Es-Salaam. Pembeni kushoto kwa Rais Chisano ni maafisa wanaohudhuria mkutano huo.
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano wa jukwaa la kujadili uchumi wa dunia kwa Afrika (World Economic Forum) unaondelea Jijini Dar-Es-Salaam. Katikati ni Waziri wa Biashara na Kilimo na usafirishaji na wa kwanza kulia ni Joe Nyagah ambaye ni Waziri wa maendeleo ya ushirika.
Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa akitoa ufafanuzi wa hoja za waandishi wa habari kwenye mkutano wa kimataifa wa kujadili uchumi wa dunia kwa Bara la Afrika jijini Da-Es-Salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu wa Eithiopia Meresi Zenawi.
Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe Profesa Arthur Mutambara akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye mkutano wa jukwaa la kujadili uchumi wa dunia kwa Afrika unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar-Es-Salaam.
Rais wa Msumbiji Armando Guebuza akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa mkutano wa jukwaa la kujadili uchumi wa dunia kwa Afrika unaondelea Jijini Dar-Es-Salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment