WAARABU WA HARAS EL HADOOD WAPAGAWA BAADA YA SIMBA KUWASILI!!

Wachezaji wa Simba wakishuka kwenye basi baada ya kuwasili jijini Alexandria wakitokea Cairo leo wanapambana na Haras El Hadood ya huko.


Habari zilizotinga ndani ya FULLSHANGWE asubuhi hii zinasema baada ya Timu ya Simba kuwasili jijini Alexandria nchini jana mchana ikitokea Cairo ilikokuwa imepiga kambi waarabu wa Haras El Hadood wameripotiwa kupagawa na kuwasili kwa timu hiyo ya wekundu wa msimbazi muda mfupi tu kabla ya pambano lao linalopigwa leo jijini humo.

Mdau wa FULLSHANGWE aliyepo katika msafara huo amenyetisha kwamba waarabu hao walitaka timu ya Simba iwahi ili waweze kufanya mipango mbalimbali kwa ajili ya maadalizi ya mchezo huo.

Lakini kwa kitendo cha Simba kuwastukiza kimewatia wazimu kwani hawajapata hata muda wa kuangali mazoezi yao na hasa pia wakikumbuka kilichowapata Zamalek mwaka 2003 hivi ni vitu vinavyozidi kuwatia mashaka waarabu hao wakati watakapokutana katika mchezo kombea la shirikisho CAF unaotarajiwa kupigwa jioni ya leo

Mdau wa FULLSHAGWE anaendelea kusema kwamba timu iko katika morali ya ushindi na hakuna hata mchezaji mmoja ambaye ni majeruhi hivyo mpaka sasa kwa asilimia 75 timu ya Simba inawea kuwafunga waarabu hao au kuwaondosha kwenye mashindano kwa tofauti ya magoli.

Mdau wa FULLSHANGWE tutakukuletea habari na matukio ya huko kadiri tutakavyaonasa kabla ya mchezo na baada ya mchezo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment