
Uongozi mpya wa simba ukiwa katika picha ya pamoja jana baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi huru na haki uliofanyika jana kwenye bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es salaam ambapo mwenyekiti alichaguliwa Ismail Aden Rna makamu mwenyekiti alichaguliwa Geofrey Nyange Kaburu Perez.

Mwenyekiti mpya wa Simba Ismail Aden Rage kulia na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu (Perez) wakipongezana mara baada tya kuibuka kidedea na kuwa viongozi wapya wa juu katika klabu ya Simba katika uchaguzi uliofanyika jana jijini Dar es salaam.

Aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa klabu ya Bw. Hassan Hasanoo akimpongeza mgombea mwenzie Ismail Aden Rage mara baada ya kutangazwa mshindi na kamati ya uchaguzi ya Simba katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es salaam.

Walioendesha uchaguzi wa kihistoria wa klabu ya Simba kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF Alex Mgongolwa na mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Simba Deo Ndumbaro

Wadau Nick Magarinza kulia na Mashaka Penza wakipiga kura kuchagua viongozi.

Kutoka kulia ni Ismail Adeni Rage Hassan Hasanoo (Mpiganaji) na Geofrey Nyange Kaburu (Perez) wakipiga kura zao.

Wagombea wa nafasi zote wakiwa wamekaa kabla ya kuanza kujieleza mbele ya wanachama.

Wanachama wa klabu ya Simba wakiendelea kujisajiri kwa ajili ya kuchagua viongozi wao.

Wanachama walijisajiri kwa teknologia ya kisasa kwani majina yao yaliingizwa kwenye kompyuta.

Mistari ya wanachama ilikuwa ni mikubwa kitu kinachoashiria kwamba kama uchaguzi usingefanyika wanachama hao wengi wabngenyimwa haki yao ya msingi.

Msururu wa wanachama wa klabu ya Simba wakiwa kwenye mstari tayari kwa kujisajiri kwa ajili ya kupiga kura jana.
0 comments:
Post a Comment