Kijana Hamis Hamad Mnondwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya nia yake ya kumvaa mbuge Abdallah Kigoda wa Handeni kupitia chama cha Mapinduzi CCM ili kuchukua jimbo na kuanza kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
Amesema wananchi wa Handeni hawahitaji kutawaliwa ila wanahitaji kuongozwa kwa kushauriana katika kuleta maendeleo ya jimbo hilo ambao liko nyuma sana kiuchumi, kielimu na kiafya pia, ameongeza kuwa yuko tayari kwa kuwatumikia wananchi wa Handeni kinachotakiwa ni wao kumuidhinisha ili aweze kuwatumikia
Amesema utaratibu uliotangaza na chama cha mapinduzi CCM unasema fomu zitaanza kutolewa kwa wagombea tarehe 26 mwezi julai na kurudishwa tarehe 28 mwezi huohuo, Hamis Hamad Mnondwa aliongozana na baba yake mzazi katika mkutano huo anayejulikana kwa jina la Njama Issa Mnondwa aliyeko kulia.
1 comments:
Inapotokea kwa kijana kama huyu kujitokeza katika masuala ya kuwakilisha wananchi katika serikali, ni muhimu kwa kila Mtanzania na familia kwa ujumla kumpa ngvu na moyo katika kuliendea jambo hilo.
Watanzaniauache kasumba ya kuwa uongozi katika nchi hii ni wa familia moja tu.Kigoda ameifanya wilaya ya Handeni kuwa ni ya familia yake tu. Hakuna kinachoendelea wala kusikika akiwatetea wananchi wa Handeni. Yapo mambo ya msingi yeye kama Mbunge kuyasema na kufuatilia lakini yuko kimya, sijuwi ni kwa maslahi ya nani, jaribu kutembelea Handeni mjini na angalia hiyo inayoambiwa kuna barabara ya kiwango cha lami, na finishing ya zoezi hilo kwa ujumla, hivi hawa viongozi wamelala au???? jamani mambo haya yataisha lini??? kila kitu kiwe ni chenye kurudiwa kila baada ya miaka kadhaa, hivi tunajenga nchi au????
Tuabadilishe huu uongozi, itakuwa ni changamoto kwa maisha ya baadae!!!
Post a Comment