JIKHOMAN KUZINDUA (TUPENDANE) DAR. NA MAGAMOYO!!

Jikhoman akipozi kwa picha mara baada ya kuzungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE jijini jana habari kamili chini.
Muonekano wa (Cover) Sura ya mbele ya Albam ya (Tupendane) ya Jikhoman ilivyo.

Jikhoman akifanya vitu vyake jukwaani.

Jikhoman akitunbuiza katika moja ya matamasha makubwa ambayo amewahi kutumbuiza na kundi lake hapa ilikuwa tamasha la ZIF Zanzibar

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa Regge hapa nchini JikhoMan anatarajiwa kuzindua Albam yake mpya inayoitwa (Tupendane ) yenye nyimbo kumi tarehe 17 Disemba mwaka huu mjini Bagamoyo kwenye ukumbi wa Tasuba, JikhoMan amesema akizindua mjini bagamoyo atakuja kufanya uzinduzi mwingine jijini Dar es alaam katika ukumbi wa nyumba ya Sanaa ambao utafanyika tarehe 21 Disemba pia.
Jikho Man ameongeza kuwa alianza kuandaa Albam hiyo toka mwaka 2007 mpaka alipoikamilisha kurekodi nchini Finland katika jiji la Helsinky kwenye Studio za StudioRed zilizopo nchini humo, anasema kuwa katika Albam hiyo ameshirikisha wanamuziki wengi wa muziki wa Regge na wengi wao ni wazungu lakini nyimbo zote zimeimbwa katika lugha ya Kiswahili yaani lugha ya nyumbani Tanzania.

Jikho man ambaye kwa sasa amejizolea sifa nyingi katika muziki huo hapa nchini anachukuliwa kama mwanamuziki pekee hazina kwa sasa hapa nchini katika muziki huo ambaye anauendeleza vyema muziki wa regge na kuupiga kwa uwezo mkubwa na ubunifu wa hali ya juu.

Anawataja wanamuziki ambao ameshirikiana nao katika katika kupiga vyombo kuimba na kutayarisha mpaka kukamilisha Albam hiyo kuwa ni A-Aroy, Antti Kana, Arvey Garwey, Cathrine, Eero Savela, Eleonora, Erno Haukkala,Heikki Tuhkanen, Jikhoman mwenyewe Micho Dread, Mikey Mike, Saara, Teho, U-Stics, Ville hoyvonen Ville Melody,Sagatti Graphic Ltd na mpiga picha Eirik Folkedal pia albam hiyo ilikuwa chini ya uratibu wa Afrkakabisa Produtions

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. jamani wacha niwe wa kwanza kutoa comment humu naona hakuna aliyetoa ila mi kwa upande wangu ndo kwanza leo nimeijua hii blog kupitia bongo celebrity.
    Pearl

  2. Na mimi niwe wa pili kutoa maoni humu.Nimekutana na blog hii kama zali kupia google.Blog ni nzuri.
    All di best man.
    Stephen-Shinyanga.

Post a Comment